MAREKANI KUENDELEZA UTEKELEZAJI WA MRADI KUBWA WA UMEME ZANZIBAR
Marekani imeelezea azma yake ya kuendeleza utekelezaji wa mradi mkubwa wa umeme kutoka Dar es salaam hadi Zanzibar kuwa iko pale pale huku juhudi zikichukuliwa katika kuhakikisha mradi huo unakamilika hapo mwakani.
Akizungumza jana na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohd Shein Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt, amesema mradi huo utakamilika hapo mwakani licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza.
Amesema mbali na mradi huo serikali ya Marekani itaendelea kuunga mkono juhudi za kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo nchini ikiwa ni pamoja na mradi maalum wa kusaidia kilimo cha umwagiliaji maji na mboga mboga.
Amesema marekani imekusudia kuanzisha programu maalum ambayo ambayo inalenga kusaidia nyenzo za kilimo na lishe bora kwa akina mama na watoto pamoja na mradi wa kusambaza kompyuta kwa kwa wanafunzi na walimu katika skuli za msingi ili kuimarisha sekta ya elimu.
Kwa upande wake Rais Shein amesema serikali inathamini juhudi zinazochukuliwa na marekani katika kuimarisha miradi ya maendeleo ukiwemo ukiwemo mradi huo mkubwa wa umeme ambao utakuwa ni suluhisho la tatizo la umeme nchini.
Amesema mbali na kuimarisha sekta ya kilimo tayari serikali imeshapitisha sera juu ya uhifadhi wa chakula hatua ambayo itasaidia kuongeza uzalishaji pamoja na uhifadhi wa chakula.
No comments:
Post a Comment