Wednesday, 16 March 2011

Polisi wazuia maandamano Dar

 

Jeshi la Polisi limesitisha maandamano yaliyokuwa yafanywe leo na Kamati ya Vijana Watanzania na wapenda amani ili kupunguza usumbufu na msongamano wa Barabara ya Morogoro iliyokuwa itumike kufanyika maandamano hayo.
Hata hivyo, jeshi hilo limeruhusu vijana hao kufanya mkutano wa kuunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya mwezi uliopita kuhusu amani nchini na kupinga hisia za kuvuruga amani hiyo, katika viwanja vya Bakharesa, Manzese jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Fulgence Ngonyani, alisema, jeshi hilo limezuia maandamano hayo baada ya kupokea barua ya maombi kutoka kwa vijana hao.
Alisema maandamano hayo yalikuwa yafanyike kuanzia Mnazi Mmoja hadi Manzese ambapo wangetakiwa kutumia barabara ya Morogoro hali ambayo ingesababisha usumbufu na foleni kwa watumiaji wa njia hiyo.

No comments:

Post a Comment