Thursday, 3 March 2011

NCHINI LIBYA: MAPIGANO MAKALI KATI YA WAASI NA VIKOSI VYA GADDAFI

Libyan leader Moamer Kadhafi speaks at a ceremony of loyalists to mark 34 years of "people power" in Tripoli on March 2, 2011 during which he vowed to fight an uprising against his 41-year rule to "the last man, the last woman", as rebels repulsed an attack by his forces on an eastern town. AFP PHOTO / MAHMUD TURKIA
Vikosi vya waasi vimefaulu kuzima juhudi za wanajeshi watiifu kwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi la kutaka kuziteka ngome mbili za waasi hao mashariki mwa nchi hiyo.

Mapigano makali yameripotiwa katika mji wa al Brega, eneo ambalo vikosi vinavyomtii Kanali Gaddafi kwa muda mfupi vilikiteka kituo kimoja cha mafuta kilichokuwa kikidhibitiwa na waasi mjini humo ambapo pia mji ulio karibu wa Adgdaabeeyah umeshambuliwa. Msemaji wa waasi wanaodhibiti sehemu kubwa ya mashariki mwa Libya Hafiz Ghoga, ameutaka Umoja wa Mataifa uongoze mashambulio ya angani dhidi ya Libya.
Wakati huo huo akizungumza mjini Tripoli Kanali Gaddafi amesema maelfu ya watu watakufa iwapo Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO itaingilia kati mzozo unaoendelea nchini Libya. Kwa upande mwingine Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)iliyopo The Hague nchini Uholanzi, imesema inaanza kuchunguza mgogoro unaofukuta nchini Libya.

KATIKA HATUA NYINGINE

Umoja wa Ulaya umeongeza msaada wa dharura hadi kufikia Euro milioni 10kwa ajili ya wakimbizi waliolazimika kuikimbia Libya. Rais wa Umoja huo Jose Manuel Barroso, amesema fedha hizo zinakusudiwa kutumika kununua vifaa vya matibabu, mahema na magodoro, huku akisema kwa sasa Libya inakabiliwa na janga la kibinadamu na kumtaka kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Ghaddafi ajiuzulu.

Naye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema Ujerumani itatoa Euro milioni moja kuwasaidia wakimbizi takriban 14,000 waliokwama kwenye mpaka kati ya Tunisia na Misri.
Sambamba na hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Seneti la Marekani inayohusika na mahusiano ya nchi za Nje Bw. John Kerry, amesema Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kuwa tayari kutekeleza marufuku ya safari za ndege katika anga ya Libya, ili kuzuia mashambulio ya Kanali Gaddafi dhidi ya wananchi wake.

No comments:

Post a Comment