Thursday, 17 March 2011

CUF yaishtukia Serikali ya Muungano suala la mafuta

 
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Ismail Jussa Ladhu

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kimeshangazwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwa wazito katika kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano, wakati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshaamua kuliondoa suala hilo.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Ismail Jussa Ladhu, katika mkutano wa kukabidhi milango ya vyuma itakayowekwa katika nyumba za maendeleo Michezani kwa ajili ya kuzilinda nyumba hizo na wahalifu.
Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliamua suala la mafuta na gesi asilia kuliondoa katika mambo ya Muungano baada ya kupata baraka za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka vyama vya CCM na CUF.
“Inashangza serikali ya Muungano hadi sasa wamekuwa wazito kuwasilisha muswada wa sheria wa kulindoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano,” alisema Jussa ambaye pia ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe.
Alisema kitendo hicho kinachelewesha harakati za Zanzibar kufanya utafiti na uchimbaji wa mafuta katika eneo la mwambao wa bahari ya kisiwa cha Pemba, sehemu ambayo inapewa matumaini makubwa ya kuwepo mafuta na gesi.
Alieleza kwamba hivi sasa ni mwaka wa pili tangu hatua hiyo kufikiwa na serikali tangu wakati wa uongozi wa Rais mstaafu, Amani Abeid Karume.
Hata hivyo, alisema wakati suala la mafuta na gesi asilia likiwa halijapatiwa ufumbuzi, Serikali ya Muungano imekuwa ikiendelea kufanya utafiti na gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia Shirika la Maendeleo ya Mafuta nchini (TPDC).
Suala la mafuta na gesi asilia liliondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano kufuatia maamuzi y
  

No comments:

Post a Comment