Vigogo Zanzibar Wafutiwa Vibali vya Ardhi
WAKATI mtandao maarufu wa WikiLeaks ukionesha harufu ya rushwa kwenye ugawaji wa ardhi ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baadhi ya mawaziri na vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameanza kufutiwa vibali vyao vya kumiliki ardhi katika maeneo mbali mbali visiwani hapa.
Tayari zaidi ya mawaziri watano ambao miongoni mwao wanaendelea na nyadhifa hizo ambao wanadaiwa kujimilikisha maeneo ya ardhi katika eneo mbali mbali wamefutiwa vibali vyao kutokana na kutofuata taratibu za umiliki wa ardhi hizo.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imeamua kulivalia njuga suala la migogoro ya ardhi na kuhakikisha wananchi wote walionyanganywa ardhi zao wanarejeshewa na waliojimbikizia viwanja bila ya kufuata taratibu wananyanganywa.
Hayo yamebainika siku chache baada ya Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi kufanya ziara katika jimbo lake la Kitope Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo alikemea baadhi ya viongozi wanaojihusisha na kupora ardhi kinyume cha sheria.
Pamoja na hilo alitishia kuwafukuza kazi wafanyakazi wote wa serikali ambao watabainika kuhusika katika migogoro ya ardhi wakiwemo masheha ambao wanatajwa sana kuhusika moja kwa moja na migogoro hiyo.
Migogoro ya ardhi Zanzibar imekuwa kwa kiasi ambacho wananchi wengi wamepoteza imani na serikali baada ya kuona malalamiko yao ya kuporwa ardhi hutoshughulikiwa huku baadhi ya watendaji wakitumia mwanya huo kujigawia viwanja na kuviuza kwa matajiri na wawekezaji bila ya kufuata sheria na taratibu za ugawaji wa viwanja.
Hivi sasa serikali imeamua kushughuilikia suala hilo ambalo la migogoro ya ardhi linadaiwa kukuwa kwa kiasi kikubwa ambapo Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora nchini katika ripoti yake ya mwaka huu imesema kitendo cha kuwanyakulia wananchi wanyonge ardhi yao ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu unaofanywa na watu wenye uwezo wakiwemo watendaji serikalini.
Licha ya kuwa baadhi ya migogoro huwa hairipotiwi katika taasisi husika lakini kulingana na takwimu za kituo cha huduma za sheria Zanzibar zaidi ya migogoro 177 ya ardhi imeripotiwa katika kituo hicho, kwa mwaka huu wa 2010 unapomalizika, na mahakama ya ardhi Zanzibar imepokea malalamiko zaidi ya 150 kwa Unguja pekee.
Baadhi ya viongozi wa serikali wanadaiwa kuhusishwa na suala la uporaji ardhi katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba kwa kutumia kisingizio cha ardhi ni mali ya serikali hivyo wametumia mwanya huo kujimegea maeneo ya ardhi hasa katika maeneo ya fukwe ambayo hupendezewa na watalii kujenga mahoteli makubwa.
Mara kadhaa kumekuwepo malalamiko ya wananchi wanyonge wakilalamikia kuchukuliwa maeneo ya ardhi ambayo aidha wamerithi kutoka kwa wazazi wao au wengine wakiwa na hati miliki zinazokubalika za kumiliki ardhi lakini baadhi ya masheha wamekuwa wakidaiwa kugawa na kuuza ardhi hizo kwa wanasiasa, matajiri na wawekezaji bila ya kufuata taratibu na sheria za ardhi zilizopo.
Zanzibar ambayo ina eneo dogo la ardhi inadaiwa viwanja vingi kuchukuliwa na matajiri, wanasiasa na wawekezaji na kuwaacha wananchi wanyonge wakilalamika kutokana na kuporwa ardhi yao ya kilimo na mifugo huku makaazi yao yakiwa ya shida kutokana na maeneo mengi hususan ya ukanda wa pwani kununuliwa na wawekezaji kwa ajili ya kujenga mahoteli ya kitalii.
Kama ilivyo Unguja maeneo mengi ya ukanda wa pwani yanadaiwa kuhodhiwa matajiri kinyume na sheria halikadhalika huko Pemba nako hakujasalimika na hilo ambapo wananchi wametishia kuandamana baada ya kutolipwa fidia walioahidiwa baada ya maeneo yao ya kilimo na ufugaji kuchukuliwa na serikali.
Hivi karibuni Waziri wa Nchi afisi ya Makamu wa pili wa rais, Mohammed Aboud Mohammed alifika Kisiwani Pemba kufuatilia sakata hilo na malalamiko ya wananchi ambao wanadai kulipwa fidia na maeneo yao .
“Ni kweli mimi nilitumwa kwa ajili ya kufuatilia suala la migogoro ya ardhi huko kisiwani Pemba na tumewasilikiza maoni yao na yatari tumeshaandika mapendekezo serikalini bila ya shaka yatafanyiwa kazi.” alisema Aboud.
Nayo Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, imejitutumua kwa kufuta vibali vya viwanja 20 ambavyo baadhi yao walimilikishwa vigogo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makaazi.
Kufutwa kwa vibali hivyo inatokana na kuwa viwanja hivyo vipo kwenye maeneo ya wazi ambayo hayaruhusiwi kujengwa kwa ajili ya makaazi ya watu.
Eneo lililofutwa vibali hivyo ni maarufu kwa jila la Mombasa kwa kwa Mchina ambapo inadaiwa waliogaiwa viwanja hivyo walikusudia kujenga maduka pamoja na ujenzi wa nyumba katika maeneo hayo ambapo idadi kubwa ya waliopewa ni mawaziri wa serikali na wafanyabiashara maarufu.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwananchi Jumapili umegundua kwamba baadhi ya wamiliki waliopewa viwanja hivyo tayari wameshaviuza kwa watu wengine.
Miongoni mwa waliofutiwa viwanja hivyo ni ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz ambaye alinukuliwa na gazeti la kila siku la Zanzibar juzi akisema ni kweli amepata hiyo barua ya kufutiwa kibali chake.
Alisema katika barua aliyopokea kutoka Idara ya Ardhi, alitakiwa kuwasilisha hati za warka waliopewa ndani ya kipindi cha wiki moja, ambapo alidai kwamba taayri ameshatekeleza amri hiyo.
“ Hilo ni kweli kiwanja nilichomilikisha kimefutwa kibali, na nimepokea barua ya kufutwa kibali tokea Novemba Mosi mwaka huu”,alisema Naibu Ferouz alipozungumza na gazeti hilo .
Aidha katika barua hiyo ya idara ya ardhi imeeleza sababu za kufutwa kwa vibali vya viwanja ni kwamba eneo hilo lina shughuli nyengine ambapo kwa mujibu wa barua shughuli hizo hazikuelezwa ni zipi.
Sababu nyengine zilizoelezwa katika barua hiyo ni kwamba kufutwa kwa vibali hivyo kutokana na kuwa eneo hilo ni la wazi na halistahili kujengwa aina yoyote ya ujenzi wa makaazi wala maduka kama ilivyo hivi sasa ambapo baadhi ya maduka yameshafunguliwa na yanaendelea na shughuli zake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Nishaji na Maji, Mwalim Ali Mwalim, alithibitisha kufutwa kwa vibali ikiwemo eneo la Mombasa Mjini ambapo vigogo hao wanadaiwa kuwa na viwanja hivyo.
Katibu huyo hakuweza kuelezea sababu za msingi juu ya hatua hiyo ya Serikali, na kueleza kuwa suala hilo limo katika Mamlaka ya Waziri na hawezi kujua chochote kinachoendelea.
“Kisheria Waziri amepewa mamlaka na uwezo wa kufuta kibali cha mtu yoyote na suala hilo ni vyema angeulizwa yeye mwenyewe”,alisema Katibu huyo alipoongea na gazeti la serikali.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini pia kuna kamati maalumu inaundwa kuchunguza nyumba za maendeleo za michenzani ambazo zinadaiwa kumilikishwa kinyume na sheria ambapo baadhi ya vigogo wa serikali wamejichukulia zaidi ya nyumba fleti tano mtu mmoja.
Sakata la ardhi na ugawaji mbaya wa rasilimali ya ardhi limekuwa likiibuka mara kwa mara ambapo katika awamu iliyopita iliwahi kuunda timu ya kuchunguza ugawaji wa viwanja eneo la Tunguu ambapo baadhi ya vigogo wa serikali wakiwemo mawaziri walipatikana kumiliki viwanja zaidi ya 7 mtu mmoja.
Suala la uporaji ardhi Zanzibar ni nyeti na limekuwa likiogopwa kuripotiwa kutokana na vigogo wakuu wa serikali kudaiwa ndio wahusika wakuu wa sakata hilo ikiwemo nyumba kubwa jambo ambalo limewatia khofu waandishi wa habari kuripoti baada ya mwandishi moja wa habari kufunguliwa kesi mahakamani kutokana na kuripoti matukio kama hayo.
Kuna kundi moja maarufu lijulikano ‘hapa pangu linadaiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa na unyakuaji wa maeneo ya ardhi huku waziri mwenye dhamana ya ardhi aliyehamishiwa wizara nyengine hivi sasa akitajwa sana kufumbia macho malalamiko ya wananchi juu uporaji wa ardhi zao.
Kutoka Zanzibar Yetu

No comments:
Post a Comment