Wednesday, 15 December 2010

UN kusaidia TZ dola 773 milioni za Marekani

 
Mwandishi wetu

SERIKALI  ya Tanzania na Umoja wa Mataifa (UN) ,wamesaini makubaliano ya utaratibu mpya wa misaada unaojulikana kama UNDAP  utakaodumu kwa miaka 4  kuanzia mwaka ujao  wenye thamani ya dola 773 milioni za Marekani.

Makubaliano hayo yalifanyika jana, jijini Dar es Salaam ,baina ya serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa , ukiwa na lengo la  kuondoa umasikini nchini kwa kusaidia Mfuko wa  mkukuta na mkuza.


Hii ni mara ya kwanza serikali ya Tanzania na UN kufikia hatua ya kusaini makubaliano hayo ikiwa ni sawa na mkataba kati ya nchi ya Tanzania na UN kwa miaka minne.

Tukio hilo lilishuhudiwa na msaidizi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Khijjah na  Alberic Kacou, kutoka UN jijini Dar es salaam.

Khijja alisema kuwa serikali ya Tanzania iko tayari  kufanya kazi na UN na kweli ni kwamba kuna UN tu na si nyingine .

 Alisema Tanzania haikuwa nyuma bali inajitahidi kupiga hatua kibiashara na huu mkataba unaonyesha ni namna gani Tanzania ilivyodhamiria kupiga hatua kimaendeleo.

Akizungumza kwa niaba ya  wawakilishi wa Umoja wa Mataifa  ,Balozi wa Ireland, Lorcan Fullam, alitoa pongezi kwa  muungano huo wa serikali ya Tanzania na  Umoja wa Mataifa akifafanua kwamba kinachoangaliwa zaidi  ni nini kitafanyika kwa hiyo miaka minne ijayo kwa sababu sio mbali.

No comments:

Post a Comment