Friday, 17 December 2010

Tido Mhando Atemwa TBC



  Tido Mhando
--------------

Habari  Hii na Sadick Mtulya na Patricia Kimelemeta

BAADA ya kufanya kazi nzuri ya kuboresha matangazo na uendeshaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC),serikali imeamua kuachana na mkurugenzi wa chombo hicho, Tido Mhando baada ya mkataba wake kuisha, lakini mtangazaji huyo maarufu ameielezea uamuzi huo kuwa kuwa ni wa utata.
Kuenguliwa kwake kumefanyika takriban miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao TBC iliripoti kwa kina na bila kupendelea chama chochote na hivyo kujivunia sifa kemkem kutoka kwa watazamaji wa TBC1 na wasikilizaji wa redio hiyo ya umma.

“Hatua hii imenishtua kidogo na hata hivi ninapoongea na wewe wafanyakazi wengi wamepata mshtuko na wengine wanalia,” alisema Tido alipoongea na Mwananchi jana. “Ni juzi (Jumatatu) ndio niliandikiwa barua na serikali ya kutakiwa kuondoka…ilikuwa kinyume kabisa na uratatibu wa serikali.“Barua ya kutakiwa kuondoka niliipata mara baada ya kukutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana , Seti Kamwanda.’

Tido, ambaye kabla ya kujiunga na TBC alikuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC), alisema kwa mujibu wa taratibu mfanyakazi anayemaliza mkataba wake anatakiwa kujulishwa suala hilo miezi sita kabla.

"Kimsingi (barua) hukumbusha kwamba mkataba unamalizika na kama serikali inakusudia kuuendeleza au la. Sasa hilo halikufanyika kwangu," alisema.

Kwa mujibu wa Tido, hatua hiyo inaweza kutafsiriwa tofauti na wananchi hasa ikizingatiwa kwamba imefikiwa miezi miwili tu tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.Wafanyakazi walipata taarifa ya kuondolewa kwa Mhando jana baada ya mkurugenzi huyo kubandika tangazo la kuwataarifu kuwa anaondoka na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Joe Rugabaramu

No comments:

Post a Comment