Wednesday, 15 December 2010

Shina Jipya la CCM lafunguliwa Rasmi Luton Uingereza

CCM – UK YAFUNGUA SHINA JIPYA LUTON UINGEREZA 
Viongozi katikati waliokaa M/kiti Tawi UK MAINA OWINO kulia mwenye kofia ABRAHAM SANGIWA Katibu wa shina jipya Luton na kulia M/kiti shina jipya Luton ALBERT NTEMI na Wliosimama toka kulia mwenye kofia Mjumbe shina jipya SAMMY MARTIN,na  JOHN MBWETE then KELVIN KISHE Mjumbe wa London paomoja na Dr.FRANK MUHIZA London
 
----
Watanzania wengi walifurika Jiji la Luton Uingereza na kujiunga na chama cha mapinduzi katika ufunguzi wa shina jipya la Luton uliofanyika siku ya Jumapili Tarehe 12. 12. 2010  katika hoteli maarufu Chiltern UK.
Wengi wao wasema wana imani kubwa na CCM katika kuiongoza Tanzania kwa kuonyesha mwelekeo wa kuwa na imani na Vijana wasomi  wachapakazi walioko ndani na nje ya nchi. 

Ufunguzi huo ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa Tawi la CCM –  UK Ndugu MAINA OWINO kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama akiwemo Katibu Uenezi wa siasa Bwana Moses Katega. Pia Viongozi kutoka mashina ya Reading, Birmingham na Sehemu zote za London walijumuika pamoja.
Katika hotuba yake fupi Ndugu MAINA OWINO alitoa changamoto nyingi za mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita chini ya Uongozi wa Mwenyekiti CCM Taifa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE katika nyanja mbalimbali kama Madini,Elimu, ukusanyaji wa mapato ya serikali, waajiriwa wenye sifa za kukidhi nafasi za uongozi serikalini katika nyanja zote na  ujasialiamali kwa watanzania wanaojitafutia maendeleo bila bugudha. 

Changamoto kuhusu ushiriki wa vijana wasomi hapa UK kuingia katika mchakato wa siasa ndani ya chama  ili kuleta mabadiliko yatakayozidi kukiimarisha chama kisera, mwelekeo na kuzidi kuwaletea watanzania  maendeleo katika nyanja mbalimbali kupambana na kupambana na umasikini  yalitolewa na Katibu wa shina jipya la Luton aliyechaguliwa siku  Ndugu ABRAHAM SANGIWA na kuungwa mkono na wajumbe wote waliohudhuria ufunguzi huo
Viongozi Waliochaguliwa siku hiyo ni: 

ALBERT NTMI – MWENYEKITI
ABRAHAM SANGIWA – KATIBU MKUU
JOHN MBWETE – MJUMBE
SAMMY MARTIN – MJUMBE
NORMAN WAGE - MJUMBE

No comments:

Post a Comment