Nahodha, Kwambwa watinga UDOM
Na Pendo Mtibuche, Dodoma
SIKU moja baada ya kutokea kwa mgomo na kufanyika kwa maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na kusababisha vurugu zilizopelekea polisi kuwatawanya kwa virungu na mabomu ya machozi, Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha na yule wa Elimu na Mafunzo ya Ufusdi, Dkt. Shukuru Kawambwa wamefika chuo hapo ili kufanya mazungumzo na uongozi wa chuo na Serikali ya Wanafunzi ili kupata ufumbuzi wa tatizo lililopo.
Wanafunzi wa chuo hicho walifanya mgomo na kutaka kuandamana kuelekea katika Ofisi ya Waziri Mkuu, wakidai fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na kulalamikia uchafu wa mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. James Msekela alifika chuoni hapo na kuwasihi wanafunzi hao kuingia madarasani na kuendelea na masomo wakati matatizo yao yakishughulikiwa, lakini hawakukubali.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya uongozi wa wanafunzi na serikali ya Mkoa kushindwa kufikia muafaka, Polisi waliingilia kati na kuwatawanya wanafunzi kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha na kuwajeruhi wengine na kuwatia nguvuni ambapo wanaoshikiliwa ni pamoja na Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Bw. Leonard Singo.
Baada ya mazungumzo hayo ilielezwa kuwa litatolewa tamko ili kurudisha hali ya amani na utulivu chuoni hapo.Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrissa Kikula alisema kuwa suala hilo walishazungumza na lipo katika mchakato.
Alisema kuwa yeye kama mzazi alisikitishwa na tukio hilo na chuo hakitafungwa, hivyo wanafunzi wataendelea na masomo huku masuala yakiendelea kushughulikiwa.
Profesa Kikula alisema kuwa katika mazungmzoa na Waziri Nahodha na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, imeundwa tume ya watu watano ambayo itatoa ripoti baada ya siku tano.

No comments:
Post a Comment