Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, |
Hussein Kauli na James Magai JOPO la Majaji watano wa Mahakama ya Rufani likiongozwa na Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, limetengua uamuzi wa Mahakama Kuu uliotupilia mbali na kufuta maombi ya wazee wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaodai mafao yao. Sambamba na kutengua uamuzi huo, uliotolewa na Jaji John Utamwa Novemba 9, mwaka huu, pia jopo hilo limemuondoa Jaji Utamwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo. Kabla ya kutupa maombi ya wastaafu hao kupitia kwa mawakili wao, Jotham Lukwaro na Charles Semgalawe, waliwasilisha mchanganuo wa madai yao, wakieleza kuwa wanaidai serikali Sh2, 149,076,684, 275.80. Wastaafu hao waliwasilisha maombi hayo baada ya Jaji Utamwa kuwataka wawasilishe mahakamani hapo taarifa kamili zinazohusu takwimu sahihi za fedha wanazodai wafanyakazi hao wapatao 31,700, na kiwango ambacho tayari wamelipwa na serikali. Hata hivyo, madai hayo yalipingwa na wakili wa serikali, Gabriel Malata, kwamba sio kweli na kudai kuwa kwa mujibu wa hukumu ya makubaliano ya Mahakama Kuu ya mwaka 2005, wastaafu hao wanadai Sh117 bilioni. Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa alikubaliana na hoja za pingamizi la serikali na kufuta kabisa maombi hayo, huku akisema hayakubaliki kwa sababu hayapo kwenye kumbukumbu za awali za kesi hiyo. Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa alisisitiza kuwa, mahakama haiwezi kutoa hati ya malipo ya Sh2 trilioni kwa wastaafu hao kwa kuwa, madai hayo yako nje na uamuzi wa mahakama hiyo wa mwaka 2005 uliotolewa na Jaji Catherine Urio. Jopo la majaji hao jana, likiongozwa na Jaji Ramadhan lilitengua uamuzi wa Jaji Utamwa baada ya kufanya marejeo ya uamuzi huo na kubaini kuwapo kwa kasoro za kisheria. Kabla ya kutoa uamuzi huo, Jaji Ramadhan alitoa fursa kwa upande wa mawakali wa wastafu hao, kueleza kilio chao kutokana na uamuzi ya Jaji Utamwa na kwamba, kila upande kwenye kesi hiyo ungependa kuona inamalizika. “Mlikuwa na malalamiko mengi kwenye magazeti, kila siku ni kilio, sasa mahakama ingependa kusikia kilio chenu ni nini ili tufikie hitimisho,” alisema Jaji Ramadhan. Baada ya kupewa fursa hiyo, Lukwaro alieleza malalamiko kuhusu uamuzi wa Jaji Utamwa, ambaye alidai alikiuka baadhi ya mambo. Alidai alishindwa kusikiliza baadhi ya mambo ambayo upande wake uliwasilisha baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lilitolewa na serikali. Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Malata alipingana na maelezo hayo kwa madai kuwa, Jaji Utamwa alisikiliza hoja zote zilizotolewa na wastaafu hao na kuzijumuisha kwenye maamuzi. Baada ya mjadala huo, Jaji Ramadhan alitangaza uamuzi na kutamka: “Baada ya kusikiliza pande zote mbili, hakuna ubishi kwamba Jaji Utamwa baada ya kutoa maamuzi ya pingamizi la upande wa wastaafu, angetakiwa kusikiliza madai yaliyotolewa na upande wa walalamikaji.” Jaji Ramadhan alisema Jaji Utamwa alifanya kosa na uamuzi wake umeondolewa na kesi hiyo itachukuliwa na jaji mwingine na kwamba, sababu za kufanya hivyo zitatolewa baadaye. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Thursday, 16 December 2010
Mahakama ya Rufani yatoa ahueni wazee Afrika Mashariki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment