Friday, 6 December 2013

Lissu: Muswada wa kura za maoni ni kinyume cha Katiba

                                                                                                                                                                                                        Dodoma.Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni imetaka Muswada wa Kura ya Maoni uondolewe bungeni hadi hapo Bunge litakapofanya marekebisho ya Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa unapingana nayo.
Awali, muswada huo ulikuwa ujadiliwe katika Mkutano wa 12 wa Bunge lakini uliahirishwa kutokana na wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge wanaotoka Zanzibar kupinga vikali kura ya maoni kupigwa visiwani humo kwa kuwa tayari huko kuna sheria hiyo.
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana, Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu alisema katika Katiba ya sasa, hakuna mahali ambako kura ya maoni inatajwa.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki alisema tofauti na Katiba ya Jamhuri, Katiba ya Zanzibar imetambua kura ya maoni kwa kuitaja rasmi katika Katiba na kuiwekea utaratibu.
“Kwa maoni ya kambi ya upinzani, Serikali ya CCM inaogopa kufungua mjadala wa marekebisho ya Katiba ili kuruhusu kura ya maoni kwa hofu kuwa mjadala huo, utapanuliwa kwa kuhoji uhuru wa Tume ya Uchaguzi katika kuendesha na kusimamia uchaguzi,” alisema.
Alisema hofu ya CCM haiwezi kukubaliwa na Bunge kama sababu ya msingi ya kutunga sheria ambazo zinapingana na Katiba.
“Kwani kwa kufanya hivyo itakuwa sawa na kubariki ukiukwaji wa Katiba ambao wabunge wote tuliopo ndani ya ukumbi huu tuliapa kuhifadhi, kuilinda na kuitetea,” alisema Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni.
Awali, akiwasilisha muswada huo bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema: “Ili kuepuka mkanganyiko unaojitokeza iwapo sheria za uchaguzi zilizopo zitatumika kusimamia uendeshaji wa kura ya maoni, Serikali imeona umuhimu wa kutumia kura ya maoni kwenye mchakato wa kutunga Katiba Mpya.
“Sheria hii si ya kudumu na itafikia ukomo wake, mara tu baada ya Katiba Mpya kupatikana na haya ndiyo madhumuni makuu ya kupendekeza kutungwa kwa sheria hii ya kura ya maoni,” alisema.
Alisema mpigakura aliyesajiliwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), au Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), atakuwa na haki ya kupiga kura ya maoni.
Kamati
Kwa upande wake, Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, imeshauri muda wa kukata rufaa kuongezwa hadi siku saba badala ya tano zilizopendekezwa katika muswada huo. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pindi Chana alisema Ibara ya 45 ya muswada huo, inaweka masharti kwa kamati ya kura ya maoni ambayo haikuridhika na uamuzi wa mahakama ya chini, kuwasilisha rufaa yake ndani ya siku tano tangu tarehe iliyopata nakala ya hukumu.
Kamati hiyo pia imeshauri Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lianze kuboreshwa kwa sababu vijana wengi wamefikisha umri wa kupiga kura na hawajaandikishwa.
Chana alisema kamati inaunga mkono mapendekezo ya muswada huo kuwa kura zitangazwe ndani ya saa 72 tangu kufungwa kwa vituo vya kupigia kura.
“Kamati inashauri Serikali kuandaa vifaa vya kisasa na kuwajengea uwezo watendaji wa tume zote mbili ili waweze kumudu usimamizi wa mchakato wa upigaji wa kura ya maoni kwa weledi na umahiri wa hali ya juu,” alisema. Aidha, alisema kamati inaunga mkono mapendekezo ya muswada huo kuwa matokeo ya kura ya maoni yataamuliwa kwa kigezo cha asilimia 50 ya kura halali zilizopigwa za kuunga mkono swali la kura ya maoni kwa pande zote mbili za Muungano.
“Ibara ya 34(2) inaweka sharti la wingi wa kura halali zilizopigwa katika suala la kura ya maoni kuwa ndilo litakaloamua kuhusu kukubalika au kutokukubalika kwa katiba inayopendekezwa. Kamati inaunga mkono masharti haya kwa kuwa uamuzi wa wananchi ndiyo wa mwisho kuhusu jambo kubwa na nyeti kama la Katiba,” alisema Chana.
Wabunge Z’bar wapinga
Utaratibu wa kuwatumia masheha katika uandikishaji wa vitambulisho vya ukaazi Zanzibar umezua mjadala mkali bungeni baada ya wabunge wa CUF, kupinga kutumika katika kuwapata wapiga kura wa Katiba Mpya.
Akichangia Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni wa mwaka 2013, Mbunge wa Chakechake, Mussa Haji Kombo alitaka kufutwa kwa kipengele kinachotaka kutumika kwa Daftari la Wapiga Kura la Zanzibar katika kupiga kura za maoni kwa kuwa kitawanyima haki Watanzania ambao hawakuandikishwa kutokana na kunyimwa vitambulisho vya ukaazi na masheha.
“Msitugawe kwa kutubagua, leo hii mtu anayeandikishwa Tabora (katika daftari la wapiga kura) haulizwi kitambulisho cha ukaazi lakini wa Micheweni haandikishwi bila kuwa na kitambulisho cha ukaazi,” alisema. “Kuna danadana nyingi katika uandikishaji wa vitambulisho vya ukaazi lakini watoto wa miaka 12 wa wanachama wa CCM wameshapata vitambulisho… zoezi hili ni muhimu tutaliharibu kwa kufuata matakwa ya vyama,” alisema Riziki Omary Juma (Viti Maalumu).
Mbunge wa Mkoani, Ally Khamis Seif, alishauri kuanzishwa kwa daftari lingine la wapiga kura ambalo halitahusisha masharti ya kuwa na vitambulisho vya ukaazi ili kuwapa nafasi Wazanzibari wote kupiga kura katika mchakato huo.
“Kama mimi Sheha wangu wa Konde alininyima kitambulisho cha ukaazi kama ya Mbunge yamekuwa hayo je, Watanzania wa kawaida? Hili jambo litatuletea taabu katika maamuzi haya magumu tunayoyafanya, tuache kutumia daftari la wapiga kura la Zanzibar lile si daftari lile ni uchochezi litatuletea taabu,” aliongeza Mbunge wa Konde, Khatibu Said Haji.
Mwananchi
 Nelson Mandela dies at 95
 
 









Former South African President Nelson Mandela died peacefully at his Johannesburg home on Thursday after a prolonged lung infection. He was 95.
Mandela, the country's first black president and anti-apartheid icon, emerged from 27 years in apartheid prisons to help guide South Africa out of bloodshed and turmoil to democracy. 

"Fellow South Africans, our beloved Nelson Rohlihlahla Mandela, the founding president of our democratic nation, has departed," President Jacob Zuma said in a nationally televised address.

"Our people have lost a father. Although we knew this day was going to come, nothing can diminish our sense of a profound and enduring loss. His tireless struggle for freedom earned him the respect of the world. His humility, passion and humanity, earned him their love," he added. 

Mandela would receive a full state funeral, 

Zuma said, ordering flags to be flown at half mast.

Al Jazeera's Tania Page, reporting from outside Mandela's home in Johannesburg, said that there was a real sense of celebration in tribute to Mandela there, while world leaders were also delivering their tributes. 

People are "singing songs decicated to Mandela", said our correspondent. 


Mandela rose from rural obscurity to challenge the might of white minority apartheid government - a struggle that gave the 20th century one of its most respected and loved figures.

He was among the first to advocate armed resistance to apartheid in 1960, but was quick to preach reconciliation and forgiveness when the country's white minority began easing its grip on power 30 years later.

Mandela was elected president in landmark all-race elections in 1994 and retired in 1999.

He was awarded the Nobel Peace Prize in 1993, an honour he shared with FW de Klerk, the white Afrikaner leader who released from jail arguably the world's most famous political prisoner.

As president, Mandela faced the monumental task of forging a new nation from the deep racial injustices left over from the apartheid era, making reconciliation the theme of his time in office.

The hallmark of Mandela's mission was the Truth and Reconciliation Commission which probed apartheid crimes on both sides of the struggle and tried to heal the country's wounds. It also provided a model for other countries torn by civil strife.

In 1999, Mandela handed over power to younger leaders better equipped to manage a modern economy - a rare voluntary departure from power cited as an example to African leaders.

In retirement, he shifted his energies to battling South Africa's AIDS crisis and the struggle became personal when he lost his only surviving son to the disease in 2005.

Mandela's last major appearance on the global stage came in 2010 when he attended the championship match of the soccer World Cup, where he received a thunderous ovation from the 90,000 at the stadium in Soweto, the neighbourhood in which he cut his teeth as a resistance leader.

Charged with capital offences in the infamous 1963 Rivonia Trial, his statement from the dock was his political testimony.

"During my lifetime I have dedicated myself to this struggle of the African people. I have fought against white domination, and I have fought against black domination."



HISTORIA YA MADIBA

Wednesday, 4 December 2013

Tuesday, 3 December 2013

RAIS DKT. KIKWETE AMTEUA DR. ASHA ROSE MIGIRO KUWA MBUNGE

asha-rose-migiro
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
 
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dr. Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumanne, Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Desemba 2, 2013.
Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.
 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
3 Desemba, 2013 

Friday, 29 November 2013

Rais Dkt. Shein Azungumza na Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais

IMG_3289
 
Baadhi ya Viongozi mbali mbali wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais,wakiwa katika cha  kujadili utekelezaji wa Mpango kazi wa Wizara hiyo,wa mwaka wa fedha 2013-2014 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013-2014,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.
 
IMG_3291
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais,katika kikao cha kujadili utekelezaji wa Mpango kazi wa Wizara hiyo,wa mwaka wa fedha 2013-2014 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013-2014,katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar,(kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza  wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji,(kusho) na Katibu Mkuu  Kiongozi DSk.Abdulhamid Yahaya Mzee .

Friday, 8 November 2013

JK Ahutubia Taifa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia Taifa kupitia Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2013.

K


Thursday, 31 October 2013

SOMA KWA MAKINI SOMO MUHIMU KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI:ASIYE RAIA WA TANZANIA NI NANI?
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Maswali mengi yanaulizwa kuhusu uraia, hasa wakati huu ambapo zoezi la kuwabaini wageni wanaoishi nchini kinyume cha sheria linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, yakitaka kujua nani hasa ni raia wa Tanzania. 

Kimsingi, masuala ya uraia duniani kote yanaongozwa na falsafa kuu mbili ambazo ni Haki za Kidamu (Jus Sanguinis - The rights of blood), ambapo mtu hupata uraia kutokana na uhusiano wa kidamu na wazazi wenye uraia wa nchi husika. Hii ina maana kwamba, pamoja na mtu kuzaliwa katika nchi husika anatakiwa pia kuwa na mzazi ambaye ni raia wa nchi hiyo. Falsafa hii ndiyo inayofuatwa na nchi ya Tanzania. 

Kwa maana nyingine kuzaliwa pekee nchini Tanzania hakumpi mtu haki ya moja kwa moja ya  kuwa raia wa Tanzania, bali mtu atakuwa raia ikiwa amezaliwa Tanzania na wakati wa kuzaliwa kwake mzazi wake mmoja sharti awe ni raia wa Tanzania.

Falsafa nyingine ni (Jus Soli - The right of Soil), ambayo mtu  hupata Uraia kutokana na kuzaliwa kwake katika ardhi ya nchi fulani. Kufuatana na Falsafa hii, mtu hupata uraia kutokana na kuzaliwa katika nchi husika bila kujali uraia wa wazazi wake.

URAIA WA TANZANIA
Masuala ya uraia nchini Tanzania yanasimamiwa na Sheria ya Uraia ya Tanzania ya mwaka 1995 Sura 357 kama ilivyorejewa mwaka 2002, pamoja na kanuni zake za mwaka 1997. Sheria hii imeanisha aina tatu za uraia wa Tanzania ambazo ni;
1. Uraia wa Tanzania kwa kuzaliwa
2. Uraia wa Tanzania kwa  kurithi
3. Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi, au kujiandikisha.

Uraia wa Tanzania wa kuzaliwa:
Utambuzi wa nani ni raia wa Tanzania unazingatia vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania, yaani kabla na baada ya uhuru wa Tanganyika, kabla na baada ya Mapinduzi ya Zanzibar na baada ya Muungano wa Tanzania. Pia, mahali alipozaliwa na alizaliwa na nani kama inavyoainishwa hapa chini:

Aliyezaliwa Tanganyika kabla ya Uhuru

Mtu aliyezaliwa Tanganyika kabla ya Uhuru alitambulika kuwa ni raia wa Tanganyika wa kuzaliwa, ikiwa mmoja wa wazazi wake alizaliwa Tanganyika na anatokana na Raia wa Uingereza, makoloni yake au nchi zilizokuwa chini ya udhamini wa Uingereza

Aliyezaliwa Tanganyika baada ya Uhuru

Mtu aliyezaliwa Tanganyika baada ya Uhuru alitambulika kuwa ni raia wa Tanganyika wa kuzaliwa, ikiwa mmoja wa wazazi wake alikuwa raia wa Tanganyika.

Aliyezaliwa Zanzibar kabla na Baada  ya Mapinduzi

Mtu aliyezaliwa Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi alitambulika kuwa ni raia wa Zanzibar wa kuzaliwa.
Ila, mtu huyo hakutambulika kuwa ni raia wa zanzibar ikiwa wazazi wake walitokana na mataifa yafuatayo; Australia, Ubeligiji, Kanada, Ceylon (Sri Lanka), Ufaransa, Italia, New Zealand, Ureno, Jamhuri ya Ireland, Afrika Kusini na Marekani.

Aliyezaliwa Tanzania siku na baada ya Muungano wa Tanzania
Mtu aliyezaliwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku na baada ya Muungano, atatambulika kuwa ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa ikiwa mmoja wa wazazi wake ni raia wa Tanzania.

Mtu hawezi kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa kama wakati wa kuzaliwa kwake hapa nchini, wazazi wake wote hawakuwa raia wa Tanzania; au Baba yake ni Balozi wa nchi ya kigeni na ana kinga ya kibalozi; au mmoja wa mzazi wake alikuwa ni adui wa nchi ya Tanzania (enemy) na mtoto huyo alizaliwa katika eneo lililokuwa likikaliwa na adui.
Sheria ya Uraia ya Tanzania Sura 357 ya mwaka 1995 (R.E, 2002) ndiyo sheria pekee inayotambua sheria zote za nyuma, zilizokuwa zinasimamia masuala yote ya uraia katika vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania.

Kwa mantiki hiyo mtu yeyote ambaye alikuwa raia wa Zanzibar au Tanganyika kwa kuzaliwa, kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 25/04/1964, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kuzaliwa, mara baada Muungano.
Aidha, mtu yeyote kama hakutambulika kuwa raia wa Zanzibar au Tanganyika kabla ya Muungano, hatatambulika kuwa ni raia wa Tanzania mara baada ya muungano.

URAIA WA TANZANIA KWA KURITHI:
Raia wa Tanzania kwa kurithi ni mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania, na anatambuliwa kuwa raia wa Tanzania kutegemeana na kipindi alichozaliwa na uraia wa wazazi wake wakati wa kuzaliwa kwake kama ifuatavyo:

Aliyezaliwa nje ya Tanganyika kabla ya Uhuru

Mtu aliyezaliwa nje ya Tanganyika kabla ya uhuru (akiwa ametokana na raia wa Uingereza na Makoloni yake au himaya ya Mwingereza) alitambuliwa kuwa ni raia wa Tanganyika kwa kurithi endapo baba yake alikuwa raia wa Tanganyika.

Aliyezaliwa nje ya Tanganyika baada ya Uhuru na kabla ya Muungano

Mtu aliyezaliwa nje ya Tanganyika baada ya Uhuru na kabla ya Muungano alitambuliwa kuwa ni raia wa Tanganyika kwa kurithi, ikiwa baba yake alikuwa raia wa Tanganyika.
Sheria ya Uraia ya Tanganyika ya mwaka 1961 haikutoa fursa kwa mama kumrithisha uraia mtoto wake aliyezaliwa nje ya nchi. Hivyo mtu aliyezaliwa nje ya Tanganyika katika vipindi tajwa hapo juu hakutambulika kuwa ni raia wa Tanganyika kwa kurithi kupitia mama yake. 

Aidha, mtu aliyezaliwa nje ya Tanganyika hakutambuliwa kuwa raia wa Tanganyika kwa kurithi iwapo baba yake alikuwa raia wa Tanganyika kwa kurithi. Kwa tafsiri rahisi ni kwamba Raia wa kurithi hawezi kurithisha tena uraia huo kwa mtoto wake aliyezaliwa nje ya Tanganyika.

Aliyezaliwa nje ya Zanzibar kabla ya Muungano wa Tanzania

Mtu aliyezaliwa nje ya Zanzibar kabla ya Muungano atakuwa raia wa Zanzibar kwa kurithi endapo baba yake ni raia wa Zanzibar.
Vile vile, Sheria ya Uraia ya Zanzibar (The Zanzibar Nationality Decree, CAP 39, 1952) haikuruhusu mama raia wa Zanzibar kurithisha uraia kwa mtoto wake aliyezaliwa nje ya Zanzibar. Kwa maana nyingine, mtu aliyezaliwa  nje ya Zanzibar katika kipindi hicho hakutambuliwa kuwa ni raia wa Zanzibar kwa kurithi kupitia kwa mama yake. 

Ieleweke pia kuwa mtu aliyezaliwa nje ya Zanzibar hakutambuliwa kuwa raia wa Zanzibar kwa kurithi ikiwa Baba yake alikuwa raia wa Zanzibar kwa kurithi. Kwa tafsiri rahisi ni kwamba Raia wa Zanzibar kwa kurithi hawezi kurithisha tena uraia huo kwa mtoto wake aliyezaliwa nje ya Zanzibar.

Aliyezaliwa nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku na baada ya Muungano wa Tanzania

Mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania siku na baada ya Muungano atakuwa raia wa Tanzania kwa kurithi endapo mzazi wake mmoja ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa au kuandikishwa/tajnisi.

Ni vyema ieleweke kuwa mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania hawezi kuwa raia wa Tanzania kwa kurithi iwapo baba/mama yake ni raia wa Tanzania kwa kurithi. 

Sheria ya Uraia Sura ya 357  ya mwaka 1995 (R.E, 2002) imetoa fursa kwa mama ambaye ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, tajnisi/kuandikishwa kurithisha uraia wa Tanzania kwa mtoto wake aliyezaliwa nje ya Tanzania.

Aidha, mtu yeyote ambaye alikuwa raia wa Zanzibar au Tanganyika kwa kurithi, kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 25/04/1964 ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ile ile mara baada Muungano. 

Mtu yeyote kama hakutambulika kuwa raia wa Zanzibar au Tanganyika kwa kurithi kabla ya Muungano, hatatambulika kuwa raia wa Tanzania kwa kurithi mara baada ya muungano.

Haya yameainishwa katika Sheria ya Uraia ya Tanzania Na.6, 1995 (Sura 357, Rejeo la 2002)  kifungu cha 30.

URAIA WA TANZANIA KWA TAJNISI (NATURALIZATION)

Mtu yoyote ambae siyo raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzaliwa au kurithi anaweza kuomba uraia wa Tanzania wa tajnisi kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Sura 357 ya mwaka 1995, (R.E,2002). 

Kwa mujibu wa sheria hiyo, Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya uraia nchini (Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi), ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya kumpa au kutompa uraia wa Tanzania Mgeni mwenye sifa anayeomba uraia.

Sifa za Kuomba Uraia wa Tajnisi;

Mgeni anaetaka kuomba uraia wa Tanzania anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

(i) Mwombaji awe na umri kuanzia miaka 18 na uwezo wa kufanya maamuzi yanayokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi,
(ii) Awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muda wa miezi 12 mfululizo kabda ya kutuma maombi ya Uraia,
(iii) Katika muda wa miaka kumi kabla ya miezi kumi na mbili hiyo awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kihalali kwa muda usiopungua miaka saba.
(iv) Awe anafahamu vizuri lugha ya Kiswahili au Kiingereza,
(v) Awe na tabia njema,
(vi) Awe na manufaa kwa taifa, yaani awe alichangia na anaendelea kuchangia katika ukuzaji wa uchumi, sayansi na teknolojia na utamaduni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
(vii) Awe anakusudia kuishi moja kwa moja ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ombi lake la uraia litakubaliwa.

Taratibu za kuomba uraia wa Tajnisi.

Mgeni yeyote mwenye nia ya kuomba uraia wa tajnisi mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea anatakiwa kufuata taratibu zifuatazo;
(i) Mwombaji anatakiwa kujaza fomu za maombi ya uraia ambazo zinapatikana katika ofisi zote za Uhamiaji za Wilaya, Mikoa, Afisi kuu ya Uhamiaji Zanzibar na Makao Makuu ya Uhamiaji Dar es Salaam.

(ii) Mwombaji anatakiwa kutoa matangazo ya nia yake ya kuomba Uraia wa Tanzania mara mbili mfululizo kwenye magazeti yaliyosajiliwa Tanzania.

Mchakato wa Kushughulikia Maombi ya Uraia
Ili kuhakikisha kuwa wageni wanaopewa uraia ni wale wenye manufaa kwa Taifa, maombi yote yanapaswa kupitia na kujadiliwa katika vikao vya Kamati za Ulinzi na Usalama za:

Ngazi ya Kata au Shehia (kwa upande wa Zanzibar)
Katika ngazi ya Kata au Shehia anayoishi mwombaji, ambapo atahojiwa na maombi yake kujadiliwa na kikao hicho na hatimaye ombi lake kupelekwa ofisi ya Uhamiaji Wilaya kwa hatua zaidi.

Ngazi ya Wilaya

Katika ngazi hii, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya itajadili maombi ya uraia yaliyowasilishwa kutoka ngazi ya Kata au Shehia, hatimaye maoni na mapendekezo yake hupelekwa katika ngazi ya mkoa.

Ngazi ya Mkoa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa nayo itajadili maombi yaliyowasilishwa na kutoa maoni na mapendekezo yake kuhusiana na ombi husika na hatimaye hutumwa kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, ambaye atatoa ushauri na mapendekezo yake kwa Mhe. Waziri mwenye dhamana ya masuala ya uraia wa Tanzania kwa maamuzi.

Ombi la Uraia wa Tajnisi kwa Mwanamke aliyeolewa.
Mwanamke mgeni ambaye ameolewa na raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wowote wa uhai wa ndoa yake, anaweza kuwasilisha maombi ya uraia wa Tanzania kwa tajnisi. 

Ombi la uraia kwa mwanamke aliyeolewa linatakiwa kuwasilishwa pamoja na viambatanisho vifuatavyo;

(i)Cheti cha ndoa kilichosajiliwa na Mamlaka husika nchini
(ii) Pasipoti ya taifa lake ambayo haijaisha muda wake
(iii) Kibali cha kuishi nchini ambacho hakijaisha muda wake (Hati ya Mfuasi)
(iv) Vielelezo vinavyothibitisha kuwa mume wake ni raia wa Tanzania.

Ombi la Uraia wa Tajnisi kwa Mtoto
Sheria ya Uraia ya mwaka 1995 Sura 357 (RE 2002), inatoa fursa kwa mzazi au mlezi halali wa mtoto (asiye raia) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumuombea mtoto huyo Uraia wa Tanzania. Baada ya maombi rasmi kuwasilishwa, Waziri mwenye dhamana ya uraia anaweza kuruhusu mtoto huyo aweze kupata uraia wa tajnisi.
Waziri mwenye dhamana na masuala ya uraia nchini (Waziri wa Mambo ya Ndani) ndiye mwenye Mamlaka ya mwisho ya kutoa au kutotoa uraia wa Tanzania kwa mwombaji yoyote kwa mujibu wa Sheria ya Uraia ya mwaka 1995 Sura 357, rejeo la 2002.
Makala hii imeandaliwa na
 Timu ya Habari ya Operesheni Kimbunga -
Oktoba, 2013 

Wednesday, 30 October 2013

                          TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 
 
 
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

 

Fax: 255-22-2113425


 
 
 
 
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatatu, Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun.

Mkutano huo wa siku mbili utafanyika keshokutwa Jumatano na Alhamisi kwenye Ukumbi wa Queen Elizabeth 2 mjini London.

Miongoni mwa mambo makuu ambayo mkutano huo utazungumzia ni Serikali Uwazi na Ajenda ya Maendeleo Baada ya Mwaka 2015 wakati muongo wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millenium Development Goals) unafikia mwisho.

Masuala mengine ambayo yatazungumzwa katika mkutano ambao Rais Kikwete anaambatana na Mawaziri wake watatu ni pamoja na uwazi katika manunuzi ya umma, uwazi katika mikataba, haki ya kupata habari, uwazi katika ukaguzi wa fedha za umma, uwazi wa Serikali na vyombo vya habari, uwazi katika mikataba ya maliasili, uwazi katika maendeleo ya nchi zinazoendelea.

Mawaziri wanaoambatana na Rais Kikwete katika ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe, Waziri wa Sheria na Katiba Mheshimiwa Mathias Chikawe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar Mheshimiwa Mwinyihaji Makame.

Rais Kikwete anatarajia kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 2, 2013.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

29 Oktoba, 2013