Meli yawaka moto Dar |
Anneth Kagenda na Christina Gauluhanga, jijini KIZAAZAA kiliwakumba baadhi ya manahodha na abiria waliokuwa wakisafiri kwa meli jijini Dar es Salaam baada ya moto kuzuka ghafla kwenye meli ya Wacomoro, M.V. Trouse, maarufu kama 'Mkeze Rajab' na kusababisha hofu kubwa kwa abiria na mali zao. Tukio hilo limetokea jana saa 11 jioni wakati meli hiyo ya mizigo ikiwa imetia nanga katika bahari hiyo hali iliyosababisha shughuli za bandari kusimama. Imedaiwa kuwa meli hiyo ipo zaidi ya mwaka mmoja sasa kwa ajili ya matengenezo. Hata hivyo, chanzo cha moto huo bado hakijafahamika. Baada ya muda kadhaa magari hayo yalionekana kushindwa ndipo meli maalumu ya bandari ilipolazimika kufanya shughuli hiyo kutokana na kwamba ilikuwa ikitumia maji ya bandari hiyo hiyo. Kutokana na hali hiyo, magari ya zimamoto na kivuko kimoja kililazimika kufanyakazi ya ziada kuuzima moto huo ambao ulizua tafrani katika bahari hiyo. Wakizungumza na Dar Leo, mashuhuda wa tukio hilo wamesema moshi ulianza kutoka taratibu chini ya meli hiyo ambapo hakuna mtu aliyeweza kugundua mara moja. Mmoja wa mashuhuda hao, Grace Mloka, amesema wakati wakiendelea na shughuli zao mara walisikia mlio wa kitu kinachopasuka na ndipo walipogundua kuwa meli hiyo inaungua. “Nafikiri kuna watu walioenda kutoa taarifa kwa wahusika kwani baada ya muda mfupi tuliona vikosi mbalimbali vya zima moto vikifika kwa ajili ya kuuzima,” amesema Mloka. Zima moto ya bandari jiji pamoja na ya Manispaa zilifika kwa ajili ya kuzima moto huo na baada ya dakika 20 moto huo ulikuwa umezimwa na meli hiyo kubaki eneo hilo hilo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema wasemaji haswa wa tukio hilo ni Kikosi cha Wanamaji. |
No comments:
Post a Comment