Kabila anusurika kupinduliwa
Na Mwandishi Wetu
Rais Joseph Kabila amenusurika kupinduliwa jana katika jaribio lililoshindikana na kusababisha watu saba kuuawa.Habari kutoka Kinshasa zinaeleza jaribio la
kumpindua lilifanyika katika makazi yake na kuzimwa na walinzi wa Rais Kabila, kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC, Lubunga Bya'Ombe akiwa Kinshasa alithibitisha kumetokea taarifa hizo huku akisema watu waliohusika bado walikuwa bado hawajajulikana.
Rais Kabila aliyekuwa mkuu wa jeshi la nchi hiyo, aliingia madarakani baada ya kuuawa baba yake aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Laurent Kabila mwaka 2001.
"Tumeshuhudia jaribiwa la mapinduzi, alisema Waziri wa habari wa nchi hiyo, Bw. Lambert Mende alilieleza Shirila la habari la uingereza, Reuters na kuongeza:
"Kundi la watu wenye silaha kali lilivamia makazi ya rais. Walizuiwa kwenye kizuizi cha kwanza. Askari wetu walipambana nao, baadhi yao walikamatwa na wengine sita kuuawa."
Bw. Mende alisema hali imedhibitiwa na mamlaka za serikali zilikuwa zinachambua ili kubaini wahusika.
Hata hivyo, habari nyingine zilisema kuwa wakati wa jaribio hilo, Rais Kabila hakuwa kwenye makazi yake.
No comments:
Post a Comment