Monday, 24 January 2011

Kampuni ya ndege yapunguza nauli Zanzibar

Fredy Azzah
 

KAMPUNI  ya safari za ndege ya Precision Air imepunguza nauli  ya kwenda Zanzibar kwa asilimia 20 huku ikiongeza  safari zake kwenda visiwani humo  ili kuvutia watalii wa ndani kutembelea huko.

 Hayo yalibainishwa juzi jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni hiyo, Phil Mwakitawa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Kwa sasa , nauli yake itakuwa ni Sh60,000 kutoka Sh82,000 ya safari za awali,” alisema Mwakitawa na kuongeza kwamba ndege itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 1.30 na kutoka Zanzibar Saa 2.30 asubuhi.

, Alifafanua kuwa, shirika hilo limeamua kufanya hivyo ili kuvutia wataalii wengi zaidi na wafanyabiashara, kurahisisha safari zao, ingawa alisema bei hizo zitadumu kwa miezi mitano kuanzia sasa.

Katika hatua nyingine, alisema Watanzania kwa sasa wanatumia usafiri wa anga kwa kiasi  kikubwa kuliko miaka michache iliyopita. Pia alisema tofauti na miezi ya nyuma, Desemba kampuni hiyo ilisafirisha watu 60,000 ikilinganishwa na Novemba ambapo lilibeba watu 58,000.

 Alieleza kuwa, ongezeko hilo la abiria lilitokana na watu wengi kwenda kusherehekea sikukuu nyumbani kwao.

Katika kipindi hicho, usafiri wa mabasi nao ulikuwa wa shida  na ulisababisha  abiria wengi kulundikana kwenye vituo vya mabasi, hali iliyosababisha magari yasiyokuwa na kibali cha kufanya safari za mikoani, kupeleka abiria katika mikoa mbalimbali. mwisho

No comments:

Post a Comment